1. Wezesha usasishaji wa kiotomatiki wa programu

Mojawapo ya mambo muhimu zaidi ya kuweka rilei yako salama ni kusakinisha masasisho ya usalama kwa wakati unaofaa na kiotomatiki ili usiweze kusahau kuihusu. Fuata maagizo ya kuwezesha kusasisha programu ya kiotomatiki ya mfumo wa uendeshaji.

2. Sakinisha tor

Kusakinisha kifurushi cha torkwa Void Linux, tafadhali endesha:

# xbps-install -S tor

3. Sanidi /etc/tor/torrc

Weka faili yako ya usanidi /etc/tor/torrc katika mahali pake

Nickname      myNiceRelay  # Badilisha "myNiceRelay" iwe kitu unachopenda
ContactInfo   your@e-mail  #Andika barua pepe yako na ufahamu kuwa itachapishwa
ORPort        443          # Unaweza tumia bandari tofauti utakopotaka
ExitRelay     0
SocksPort     0
Log notice    syslog
DataDirectory /var/lib/tor
User          tor

4. Wezesha na uanzishe tor

Tofauti na usambazaji wa hivi majuzi Void Linux haitumii systemd; inatumia runit badala yake.

Kuwezesha huduma ya tor kwenye mfumo uliowashwa:

# ln -s /etc/sv/tor /var/service/.

Mara tu baada ya kuwezesha huduma itaanza moja kwa moja. Ikiwa tayari umeanzisha daemon ya tor hapo awali na ulifanya mabadiliko kufanya usanidi wake unaweza kuianzisha tena kwa:

# sv restart tor

5. Maelezo ya mwisho

Ikiwa una shida kusanidi kiungo chako angalia sehemu yetu ya usaidizi. Ikiwa kiungo chako kinajiendesha sasa tazama maelezo ya baada ya usakini.