1. Wezesha usasishaji wa kiotomatiki wa programu

Mojawapo ya mambo muhimu zaidi ya kuweka rilei yako salama ni kusakinisha masasisho ya usalama kwa wakati unaofaa na kiotomatiki ili usiweze kusahau kuihusu. Fuata maelekezo ili kuwezesha usasishaji wa programu ya kiotomatiki kwenye mfumo wako wa uendeshaji.

2. Usakinishaji wa kifurushi

Mifumo ya hivi karibuni ya OpenBSD tangu 6.5 tayari ina hazina iliyosanidiwa kwenye /etc/installurl kwa hivyo hatuhitaji kujisumbua kuibadilisha.

Ikiwa hiyo sio suala lako tafadhali rekebisha faili ya usanidi ya installurl kama hii:

# echo "https://cdn.openbsd.org/pub/OpenBSD" > /etc/installurl

Endelea na pkg_add ili kusakinisha kifurushi:

# pkg_add tor

3. Faili ya usanidi

Weka faili ya usanidi /etc/tor/torrc mahali pake:

Nickname      myNiceRelay  # Badilisha "myNiceRelay" iwe kitu unachopenda
ContactInfo   your@e-mail  #Andika barua pepe yako na ufahamu kuwa itachapishwa
ORPort        443          # Unaweza tumia bandari tofauti utakopotaka
ExitRelay     0
SocksPort     0
Log notice    syslog
DataDirectory /var/tor
User          _tor
RunAsDaemon   1

4. Badilisha openfiles-max na maxfiles

Kwa chaguo-msingi OpenBSD hudumisha kikomo cha chini kwa idadi ya juu zaidi ya faili zilizofunguliwa kwa mchakato. Kwa daemon kama vile ya Tor, ambayo hufungua muunganisho kwa kila rilei nyingine (kwa sasa ni karibu rilei 7000), mipaka hii inapaswa kuinuliwa.

Ongeza sehemu ifuatayo kwa /etc/login.conf:

tor:\
    :openfiles-max=13500:\
    :tc=daemon:

OpenBSD pia huhifadhi faili ya kikomo cha maelezo yakiwango cha kernel katika kigezo cha sysctl kern.maxfiles.

Iongeze kutoka chaguo msingi ya 7030 hadi 16000:

# echo "kern.maxfiles=16000" >> /etc/sysctl.conf
# sysctl kern.maxfiles=16000

5. Anzisha huduma

Hapa tunaweka tor kuanza wakati wa kuwasha na kuiita kwa mara ya kwanza:

# rcctl enable tor
# rcctl start tor

Ili kutumia vikomo vyetu vilivyoinuliwa vya faili zilizo wazi, hakikisha umeanza tor kwa rcctl.

6. Maelezo ya mwisho

Toleo la hivi punde la tor litafanywa kupatikana kama kifurushi cha toleo la hivi karibuni la OpenBSD na OpenBSD -current(picha ya ukuzaji), kwa hivyo, kumbuka kusasisha OpenBSD kwa wakati na kusanidi masasisho ya programu kiotomatiki.

Ikiwa unapata shida kusanidi rilei yako tazama sehemu ya msaada wetu. Ikiwa rilei yako inaendeshwa sasa angalia maelezo ya baada ya kusakinisha.