1. Wezesha usasishaji wa kiotomatiki wa programu

Mojawapo ya mambo muhimu zaidi ya kuweka rilei yako salama ni kusakinisha masasisho ya usalama kwa wakati unaofaa na kiotomatiki ili usiweze kusahau kuihusu. Fuata maagizo ya kuwezesha kusasisha programu ya kiotomatiki ya mfumo wa uendeshaji.

2. Sakinisha tor

Ili kusakinisha kifurushi cha tor kwenye Arch Linux, tafadhali endesha:

# pacman -Syu tor

3. Sanidi /etc/tor/torrc

Weka faili yako ya usanidi /etc/tor/torrc katika mahali pake

Nickname      myNiceRelay  # Badilisha "myNiceRelay" iwe kitu unachopenda
ContactInfo   your@e-mail  #Andika barua pepe yako na ufahamu kuwa itachapishwa
ORPort        443          # Unaweza tumia bandari tofauti utakopotaka
ExitRelay     0
SocksPort     0
Log notice    syslog
DataDirectory /var/lib/tor
User          tor

4. Wezesha na uanzishe tor

# systemctl enable --now tor
... or restart it if it was running already, so configurations take effect
# systemctl restart tor

5. Maelezo ya mwisho

Ikiwa una shida kusanidi kiungo chako angalia sehemu yetu ya usaidizi. Ikiwa kiungo chako kinajiendesha sasa tazama maelezo ya baada ya usakini.