Asante kwa nia yako ya kutusaidia na tafsiri. Juhudi zetu za localization zimeungwa mkono na Localization Lab.

Orodha ya barua pepe ya utafsiri

Kuwasiliana na watafsiri wengine, tafadhali jiunge na Tor localization mailing list, ambapo tunapanga tafsiri, kuchukua maamuzi, kuripoti hitilafu katika alama zinazotambua chanzo cha kutafsiri n.k. Tafadhali jitambulishe na uulize maswali yeyote unayoweza kuwa nayo baada ya kufuata maelekezo haya.

Jukwaa la kutafsiri

Juhudi zetu za localization zimewekwa katika weblate, Jukwaa la utafsiri kwa watu wengine.

Unaweza kuwasilisha mapendekezo bila kukutambulisha, lakini ni bora kufungua akaunti, ili uweze kutoa maoni na kujadiliana na watafsiri wengine, au kukagua michango yao.

Kumbuka kwamba jina la mtumiaji na anwani ya barua pepe utakayoichagua itaonekana hadharani kwenye mfumo wa tafsiri kwa kuwa yatahusishwa na mabadiliko unayoyafanya. Tunahimiza matumizi ya akaunti bandia.

Kabla ya kutafsiri, tafadhari soma kupitia ukurasa wa Tor Project kwenye Localization Lab Wiki, na nyaraka zetu katika Tor L10n wiki for translators na reviewers. Ukurasa huu unajumuisha miongozo, taarifa, na vipaumbele vitakavyo kusaidia kufaidika kutokana na mchango wako.

Kujisajili kwenye Weblate

  1. Nenda kwenye ukurasa wa kujisajili kwenye wavuti. Kumbuka kwamba jina la mtumiaji na anwani ya barua pepe utakayoichagua itaonekana hadharani kwenye mfumo wa tafsiri kwa kuwa yatahusishwa na mabadiliko unayoyafanya. Tunahimiza matumizi ya akaunti bandia.
  2. Jaza ukurasa unaofuata na maelezo yako, na usubiri barua pepe ya uthibitishaji (inaweza kuchukua hadi dakika 10 kufika kwenye kikasha chako).
  3. Washa akaunti yako kwa kubofya barua pepe kutoka kwa tovuti, kukubaliana na sheria na masharti na kuongeza nenosiri jipya.
  4. Katika ukurasa unaofuata, chagua lugha utakazotafsiri kutoka kwenye menyu, na uhifadhi.
  5. Nenda kwenye Arifa na uchague Mradi wa Tor kutoka kwa miradi inayotazamwa. Miradi mingine tunayoipendekeza ni Guardian Project na Onionshare: Tazama mradi wa Tor katika Weblate.
  6. Hakikisha pia umechagua arifa za miradi unayotazama.
  7. Sasa utaona tafsiri za Tor Project kwenye dashibodi yako ya tovuti: dashibodi ya weblate.
  8. Ili kuanza kutafsiri nyenzo mpya, kwanza unahitaji kukubaliana na 'Mkataba wake wa Mchangiaji'. Kila rasilimali ina Mkataba wake wa Wachangiaji.

Nini cha kutafsiri ya kwanza?

Ikiwa tayari kuna nyenzo za Tor zilizotolewa kwa lugha yako tafadhali anza kwa kusasisha hizo. Unaweza ona tafsiri kwa kipaumbele zaidi katika ukurasa wetu wa takwimu za tafsiri.

IRC chaneli

Tunabarizi katika chaneli ya #tor-l10n kwenye mtandao wa oftc IRC. Tafadhali jiunge nasi ili kuzungumzia ujanibishaji (l10n)! Unaweza pia kutumia Element https://element.io/ to connect: #tor-l10n:matrix.org.

Tor kila mwezi Localization Hangouts

Tunakutana kwenye chaneli yetu ya irc kila Ijumaa ya 3 ya mwezi. Njoo ili kubarizi na watafsiri wengine, kuuliza maswali, au kutafsiri kwa urahisi pamoja.