Baadhi ya lugha ni amilifu zaidi kuliko zingine zikiwa na idadi kubwa ya wachangiaji wanaofanya kazi kwa kujitolea. Hata hivyo bado unakaribishwa kutusaidia na lugha hizi hata baada ya tafsiri kukamilika.

Tafsiri zetu bado hazijakamilika katika lugha nyingi, Huenda zinazungumzwa na watu wachache duniani kote, lakini bado ni muhimu tuboreshe ufikiwaji wa Tor kwa watu ambao hawazungumzi lugha ya kingereza.

Tuko na takwimu kuhusu tafsiri zetu katikaukurasa wa takwimu wa L10n yenye maelezo kuhusu tafsiri zilizopewa kipaumbele na tafsiri zilizotolewa. Takwimu hizi huhesabiwa kila siku.

Ili kujifunza zaidi juu mafaili tofauti ya tafsiri, tafadhari omba usahuri sehemu yetu ya wiki kwa watafsiri

Unaweza kuona tiketi ziliyofunguliwa kuhusu tafsiri kwenye bugtracker.