Hongera!

Ukifika kwenye hatua hii inamaanisha kuwa kiungo cha obfs4 inaendeshwa na kusambazwa na BridgeDB kwa watumiaji waliothibitiwa. Kumbuka kuwa inaweza kuchukua siku au wiki kadhaa hadi utakapoona watumiaji wengi, kwa hivyo usivunjike moyo ikiwa huoni miunganisho ya watumiaji mara moja. BridgeDB inatumia ndoo sita kwa usambazaji wa kiungo:HTTPS, Moat, Baruapepe, Telegramu, Mipangalio na mwongozo. Baadhi ya vyombo hutumiwa zaidi kuliko zingine, ambayo pia huathiri wakati hadi kiungo chako kione watumiaji. Unaweza kwa mikono badilisha mbinu ya usambazaji wa kiungo chako. Hatimaye, hakuna watumiaji wengi wa kiungo huko nje kwa hivyo huwezi kutarajia kiungo chako kuwa maarufu kama rilei.

Ikiwa ungependa kuunganisha kwenye kiungo chako mwenyewe utahitaji kujua cheti cha kiungo cha obfs4. Tazama faili ya obfs4_bridgeline.txt ambayo inapatikana katika saraka ya Data ya Tor kwa mfano katika Debian/Ubuntu /var/lib/tor/pt_state/obfs4_bridgeline.txt au FreeBSD /var/db/tor/pt_state/obfs4_bridgeline.txt.

Au unapotumia Docker tumia amri ifuatayo kupata safu ya kiungo:

docker exec CONTAINER_ID get-bridge-line

Bandika laini nzima ya kiungo kwenye kivinjari cha Tor:

Bridge obfs4 <IP ADDRESS>:<PORT> <FINGERPRINT> cert=<CERTIFICATE> iat-mode=0

You'll need to replace <IP ADDRESS>, <PORT>, and <FINGERPRINT> with the actual values, which you can find in the tor log. Make sure to use your server's identity key fingerprint for <FINGERPRINT>, not <HASHED FINGERPRINT> or the ed25519 key; and that <PORT> is the obfs4 port you chose - and not the OR port.

Hatimaye, unaweza kufuatilia matumizi ya kiungo cha obfs4 kwenye Upekuzi wa Rilei. Ingiza tu <HASHED FINGERPRINT> ya kiungo chako katika fomu na ubofye "Tafuta". Baada ya kusanidi kiungo inachukua takriban saa tatu kwa kiungo kuonekana kwenye Utafiti wa Rilei.