Kumbukumbu: Unapaswa kunedesha kiungo cha windows ikiwa tu unaweza kuiendesha 24/7. Iwapo mwendeshaji hawezi kuthibitisha kwamba Snowflake ni njia bora ya kuchangia kwenye nyenzo.

1. Pakua Windows Expert Bundle na kivinjari ya Tor

Utahitaji kuonyesha vipengee vilivyofichwa na viendelezi vya jina la faili. Katika kichunguzi cha window, upande wa juu kushoto, bonyeza kwenye kichupo cha kutazama. Katika sehemu ya onyesha/ficha iliyo katika upande wa mwisho kabisa wa kulia, tia alama kwenye kisanduku cha kutia alama ya vipengee vilivyofichwa; tia alama kwenye kisanduku cha kutia alama kwa viendelezi vya jina la faili.

2. Tengeneza faili na uhamishe

Fungua folda ya Tor kwenye eneo-kazi lako. Bonyeza mara mbili tor.exe. Mara tu agizo la amri likisomeka: [notisi] Bootstrapped 100% (imekamilika): Imefanywa funga dirisha. Hii inaunda folda C:\Users\<user>\AppData\Roaming\tor\ (ambapo <user> ndio jina lako la mtumiaji).

Kutoka kwa folda ya Tor iliyo kwenye eneo-kazi yako, chagua .dll's and .exe zote na kuzikata na kubandika kwenye folda ya C:\Users\<user>\AppData\Roaming\tor\.

Fungua folda ya Data kwenye eneo-kazi lako. Ndani ya folda hiyo ya Tor chagua geoip na geoip6 na uzikate/uzibandike kwenye folda ya C:\Users\\AppData\Roaming\tor`.

Enda kwa C:\Users\<user>\Desktop\Tor Browser\Browser\TorBrowser\Tor\PluggableTransports. Chagua obfs4proxy.exe na Kukata/kubandika ndani ya folda ya C:\Users\<user>\AppData\Roaming\tor\.

3. Unda na usasishe faili yako ya usanidi wa Tor

Katika folda ya C:\Users\<user>\AppData\Roaming\tor\ bonyeza kulia kwenye nafasi nyeupe na uchague New > Text Document. Taja faili ya torrc; hakuna uenezi.

Bonyeza mara mbili kwenye faili ya torrc. Unapokumbusha Je, ungependa kufungua vipi faili hii? chagua Notepad. Ongeza yafuatayo:

Log notice file C:\Users\<user>\AppData\Roaming\tor\notice.log
GeoIPFile C:\Users\<user>\AppData\Roaming\tor\geoip
GeoIPv6File C:\Users\<user>\AppData\Roaming\tor\geoip6

BridgeRelay 1

# Badilisha "TODO1' na bandari ya Tor ya chaguo lako.
# Bandari hii inapaswa kufikiwa na nje.
# Epuka bandari ya 9001 kwa sababu inahusishwa kwa kawaida na Tor na vidhibiti vinaweza kuwa vinachanganua mtandao kwa bandari hiyo.
ORPort TODO1

ServerTransportPlugin obfs4 exec C:\Users\<user>\AppData\Roaming\tor\obfs4proxy.exe

# Badilisha "TODO2" na bandari ya obfs4 ya chaguo lako.
# Bandari hii lazima ipatikane nje na lazima iwe tofauti na iliyobainishwa kwa bandari ya OR.
# Epuka bandari ya 9001 kwa sababu inahusishwa kwa kawaida na Tor na vidhibiti vinaweza kuwa vinachanganua mtandao kwa bandari hiyo.
ServerTransportListenAddr obfs4 0.0.0.0:TODO2

# Bandari ya mawasiliano ya ndani kati ya Tor na obfs4. Daima weka hii kwa "otomatiki".
# "Ext" inamaanisha "kupanuliwa", sio "nje". Usijaribu kuweka nambari maalum ya bandari, wala usikilize kwenye 0.0.0.0.
ExtORPort auto

# Badilisha "<address@email.com>" na barua pepe ili tuwasiliane nawe ikiwa kuna shida na kiungo chako.
# Hii ni kwa hiari lakini inahimizwa.
ContactInfo <address@email.com>

# Chagua jina la utani unalopenda kwa kiungo chako. Hili ni la hiari.
Nickname PickANickname

Usisahau kubadalisha chaguzi yaORPort, ServerTransportListenAddr, ContactInfo, <user> na Nickname.

  • Tumia bandari ya obfs4 isiyobadilika iliyo kubwa kuliko 1034 bado ukiepuka 9001.

  • Kumbuka kuwa bandari ya Tor OR na bandari ya obfs4 lazima ifikiwe. Ikiwa kiungo chako kipo nyuma ya firewall au NAT hakikisha unafungua bandari zote mbili. Unaweza kutumia jaribio letu la kufikia kuona bandari yako ya obfs4 inafikiwa kutoka kwa mtandao.

4. Anzisha Tor

Fungua Programu ya Amri ya Shawishi. Badilisha saraka yako na cd C:\Users\<user>\AppData\Roaming\tor\. Andika: tor.exe -f torrc.

5. Fuatilia kumbukumbu zako

Ili kuthibitisha kiungo chako kinaendeshwa bila suala unapaswa kuona kitu kama hii C:\Users\<user>\AppData\Roaming\tor\notice.log.

[notice] Your Tor server's identity key fingerprint is '<NICKNAME> <FINGERPRINT>'
[notice] Your Tor bridge's hashed identity key fingerprint is '<NICKNAME> <HASHED FINGERPRINT>'
[notice] Registered server transport 'obfs4' at '[::]:46396'
[notice] Tor has successfully opened a circuit. Looks like client functionality is working.
[notice] Bootstrapped 100%: Done
[notice] Now checking whether ORPort <redacted>:3818 is reachable... (this may take up to 20 minutes -- look for log messages indicating success)
[notice] Self-testing indicates your ORPort is reachable from the outside. Excellent. Publishing server descriptor.

6. Maelezo ya mwisho

Ikiwa una shida kusanidi kiungo chako angalia sehemu yetu ya usaidizi. Ikiwa kiungo chako kinaendeshwa sasa tazama maelezo ya baada ya kusakinisha.