1. Wezesha usasishaji wa kiotomatiki wa programu

Mojawapo ya mambo muhimu zaidi ya kuweka rilei yako salama ni kusakinisha masasisho ya usalama kwa wakati unaofaa na kiotomatiki ili usiweze kusahau kuihusu. Fuata maagizo ya kuwezesha kusasisha programu ya kiotomatiki ya mfumo wa uendeshaji.

2. Sanidi pkg_add

Matoleo ya kisasa ya mfumo wa uendeshaji wa NetBSD yanaweza kuwekwa ili kutumia pkgin ambayo ni kipande cha programu inayolenga kuwa kama apt au yum kwa ajili ya kudhibiti vifurushi vya binary ya pkgsrc. Hatugeuzi usanidi wake hapa na uchague kutumia pkg_add wazi badala yake.

# echo "PKG_PATH=http://cdn.netbsd.org/pub/pkgsrc/packages/NetBSD/$(uname -m)/$(uname -r)/All" > /etc/pkg_install.conf

3. Sanikisha Tor

# pkg_add tor

4. Sanikisha proksi ya obfs4

# pkg_add install obfs4proxy

5.Hariri faili yako ya usanidi wa Tor ambayo kwa kawaida iko katika /usr/pkg/etc/tor/torrc na ubadilishe yaliyomo na:

BridgeRelay 1

# Badilisha "TODO1' na bandari ya Tor ya chaguo lako.
# Bandari hii inapaswa kufikiwa na nje.
# Epuka bandari ya 9001 kwa sababu inahusishwa kwa kawaida na Tor na vidhibiti vinaweza kuwa vinachanganua mtandao kwa bandari hiyo.
ORPort TODO1

ServerTransportPlugin obfs4 exec /usr/pkg/bin/obfs4proxy

# Badilisha "TODO2" na bandari ya obfs4 ya chaguo lako.
# Bandari hii lazima ipatikane nje na lazima iwe tofauti na iliyobainishwa kwa bandari ya OR.
# Epuka bandari ya 9001 kwa sababu inahusishwa kwa kawaida na Tor na vidhibiti vinaweza kuwa vinachanganua mtandao kwa bandari hiyo.
ServerTransportListenAddr obfs4 0.0.0.0:TODO2

# Bandari ya mawasiliano ya ndani kati ya Tor na obfs4. Daima weka hii kwa "otomatiki".
# "Ext" inamaanisha "kupanuliwa", sio "nje". Usijaribu kuweka nambari maalum ya bandari, wala usikilize kwenye 0.0.0.0.
ExtORPort auto

# Badilisha "<address@email.com>" na barua pepe ili tuwasiliane nawe ikiwa kuna shida na kiungo chako.
# Hii ni kwa hiari lakini inahimizwa.
ContactInfo <address@email.com>

# Chagua jina la utani unalopenda kwa kiungo chako. Hili ni la hiari.
Nickname PickANickname

Usisahau kubadilisha chaguo la Bandari ya OR, ServerTransportListenAddr, Maelezo ya Mawasiliano na Jina la Utani.

  • Kumbuka kuwa bandari ya OR ya Tor na bandari yake ya obfs4 lazima ipatikane. Ikiwa kiungo chako kiko nyuma ya ngome au NAT hakikisha umefungua bandari zote mbili. Unaweza kutumia jaribio letu la ufikivu ili kuona kama bandari yako wa obfs4 unaweza kufikiwa kutoka kwa mtandao.

6. Aanzisha Tor

# ln -sf /usr/pkg/share/examples/rc.d/tor /etc/rc.d/tor
# echo "tor=YES" >> /etc/rc.conf
# /etc/rc.d/tor start

7. Kufuatilia kumbukumbu zako

Ili kuthibitisha kuwa kiungo chako kinaendeshwa bila matatizo yoyote unapaswa kuona kitu kama hii (kwa kawaida katika /var/log/tor/log au /var/log/syslog):

[notice] Your Tor server's identity key fingerprint is '<NICKNAME> <FINGERPRINT>'
[notice] Your Tor bridge's hashed identity key fingerprint is '<NICKNAME> <HASHED FINGERPRINT>'
[notice] Registered server transport 'obfs4' at '[::]:46396'
[notice] Tor has successfully opened a circuit. Looks like client functionality is working.
[notice] Bootstrapped 100%: Done
[notice] Now checking whether ORPort <redacted>:3818 is reachable... (this may take up to 20 minutes -- look for log messages indicating success)
[notice] Self-testing indicates your ORPort is reachable from the outside. Excellent. Publishing server descriptor.

8. Maelezo ya mwisho

Ikiwa una shida kusanidi kiungo chako angalia sehemu yetu ya usaidizi. Ikiwa kiungo chako kinaendeshwa sasa tazama maelezo ya baada ya kusakinisha.