Vyanzo vya kisheria

Waendeshaji wa exit relay wanapaswa kuelewa hatari zinazoweza kutokea zinazohusiana na kutumia exit relay. Kwa waendeshaji wengi katika nchi nyingi, viungo na relay za guard/middle zipo katika hatari ndogo. Exits ni zile zinazowasilisha masuala fulani ya kisheria, lakini waendeshaji katika hali nyingi wataweza kushughulikia masuala ya kisheria kwa kuwa na barua ya majibu ya unyanyasishaji, kutumia exit kutoka eneo ambalo sio sehemu hayo, na kusoma kupitia baadhi ya vyanzo vya kisheria ambazo wanasheria wanaoiunga mkono tor wapo pamoja.

EFF Tor Legal FAQ hujibu maswali mengi ya kawaida kuhusu utendaji wa relay na sheria, Pia tuna Noisebridge's wiki kama nyongeza ya vyanzo vya kisheria.

kwa kawaida ni wazo zuri kushauriana na mwanasheria kabla hujaamua kuendesha exit relay, haswa ikiwa unaishi sehemu ambapo waendesha exit realy wamefanyiwa ukatili, au ukiwa wewe ni muendeshaji pekee wa exit relay katika mkoa wako. Wasiliana na shirika la ndani la haki za kidigitali kuona kama wana maependezo kuhusu msaada wa kisheria, na kama huna uhakika ni shirika gani linafanya kazi katika mkoa wako, waandikie EFF na angalia kama wanaweza kukusaidia kukuunganisha.

Pia tizama Muongozo wa Tor Exit.

Kujibu malalamiko ya unyanyasaji

Waendeshaji wanaweza kuweka kwa pamoja majibu yao ya kiolezo cha malalamiko ya unyanyasaji kutoka katika violezo vingi vya Tor vilivyo tengenezwa: Tor Abuse Templates.

Ni muhimu kujibu malalamiko ya unyanyasaji kwa muda (kwa kawaida ndani ya masaa 24). ikiwa mtumiaji akikasirishwa na kiwango cha unyanyasaji unaweza kupunguza idadi ya milango inayoruhusiwa katika sera ya kutoa data. Tafadhali andika uzoefu wako na wasimamizi wapya katika kurasa ifuatayo: GoodBadISPs

Nyaraka nyingine kama:

Kutumia relay na watu wengine

Kutumia relay na watu wengine inafurasha zaidi! Unaweza kufanya kazi na idara ya chuo kikuu, taasisi iliyokuajiri, au shirika kama Torservers.net kutumia relay.

Torservers.net

Torservers ni mtandao huru, wa kimataifa wa mashirika unaosaidia mtandao wa Tor katika uendeshaji wa relay za Tor katika usahirishaji wa data wa kiwango kikubwa.

Kuwa mshirika wa Torservers ni njia nzuri ya kujihusisha zaidi na jumuiya ya Tor relay, na itakusaidia kuunganishwa na waendeshaji wa kujitolea wa relay ulimwenguni mwote kwa ajili ya mshikamano na msaada.

Kuanzisha ushiriki wa Torservers, kitu muhimu zaidi ni kuwa na kikundi cha watu (3-5 unashauriwa kuanza nao) wenye nia ya kusaidia shughuli mbalimbali zinazohitajika kuendesha relays.

Lazima kuwa na kuaminia kati ya watu kwenye kikundi, na wanachama wanapaswa kujitoa kuendesha relays kwa muda mrefu.

Kama humjui yeyote katika mtandao wako wa kijamii anayevutiwa na kuendesha relays, sehemu moja ya watu kukutana wataalam wa teknolojia wa ndani.

Mara baada ya kuwa na kundi la watu wanaoaminika, wanaotoka ndani ya mkoa wako, mara nyingi ushauriwa kuunda aina fulani la shirika lisiloingiza faida.

Haya ni matumizi ya kuwa na akaunti ya benki, umiliki wa pamoja, maombi ya ruzuku, n.k. Katika nchi nyingi kufanya kazi kama shirika badala ya mtu wa kawaida kunaweza kukupata ulinzi fulani wa kisheria.

Hatua inayofuata ni kuitengeneza vifaa, usafirishaji wa data, na kumilikisha seva. Kutegemeana na sehemu uliopo na muunganiko ndani ya jumuiya ya kiufundi katika eneo hilo, ya mwisho inaweza kuwa hatua ngumu zaidi.

Watoa huduma wadogo wa ndani mara chache wana nafasi ya kusafirishaji data nyingi za ziada, na wanaweza kuwa wanavutiwa kusaidia kikundi chako kwa baadhi ya usafirishaji wa data nyingi au utunzaji wa data.

Ni umuhimu sana wa kuendeleza ushirikiano mzuri na watoa huduma za kimtandao.

katika chuo chako

Idara nyingi za sayansi ya kompyuta, maktaba ya vyuo, na wanafunzi wenyewe na kitivo kinachoendesha relay katika mtandao wa chuo.

Vyuo hivi ikiwa ni pamoja na Massachusetts Institute of Technology (MIT CSAIL), Boston University, the University of Waterloo, the University of Washington, Northeastern University, Karlstad University, Universitaet Stuttgart, na Friedrich-Alexander University Erlangen-Nuremberg.

Kujifunza zaidi kuhusu jinsi ya kupata msaada wa relay katika mtandao wako wa chuo, tizama vyanzo vya EFF's: Tor chuoni Part 1 - It's Been Done Before and Should Happen Again na Part 2 - Icebreakers and Risk Mitigation Strategies.

Katika kampuni au shirika lako

Ikiwa unafanya kazi katika kampuni au shiriki linalofaa kwa Tor, hipo ni mahala pazuri kuendesha relays. Baadhi ya makampuni hutumia relay ikiwa ni pamoja na Brass Horn Communications, Quintex Alliance Consulting, Private Internet Access, Boing Boing na OmuraVPN.

Baadhi ya mashirika hutumia Tor relay ikiwa ni pamoja na Digital Courage, Access Now, Derechos Digitales, Enjambre Digital na Lebanon Libraries in New Hampshire.

Relay mbovu

Relay mbovu ni ile ambayo haifanyi kazi vizuri au inasumbua katika muunganisho wa watumiaji wetu, Hii inaweza kuwa na programu iliyoharibika au haijasanidiwa vizuri. Relay mbovu nyingi zimenaswa shukrani kwa jamii yetu kubwa, hivyo tunashukuru kwa msaada wenu na uangalifu! Jifunze jinsi ya kutoa taarifa juu ya relay mbovu.

Vyanzo vingine

Hongera, wewe ni muendeshaji rasmi wa Tor relay! Sasa?

  • Unaweza kuangalia usafirishwaji wa data na takwimu zingine kwa relay yako katika Tafuta Relay (Relay yako itaonekana katika "Relay Search" ndani ya masaa 3 tangu umeanza kutafuta).

  • Pia kuna taarifa za ziada kuhusu ya kutumia relay katika Tor FAQ.

  • Na, cha umuhimu zaidi, hakikisha kutuma barua pepe tshirt@torproject.org na claim your swag. Ni njia ya kusema shukrani kwa kutetea faragha na uhuru wa kujieleza mtandaoni.

Violezo vya unyanyasaji wa Tor

Jinsi ya kushughulikia malalamiko ya unyanyasaji

Vyuo vikuu vya rilei za Tor

Je, ninawezaje kufanya Chuo Kikuu changu / mtoa huduma wa mtandao / nk kufurahishwa na nodi yangu ya kutoka?

Watoa huduma wa Mtandao wazuri wabaya

Baadhi ya watoa huduma za mtandao ni rafiki wa Tor na wengine sio

Miongozo ya Tor ya Kutoka

Utangulizi wa haraka wa kuendesha upeanaji wako wa kutoka

Madoido

Kama unaendesha rilei ya haraka au umefanya kitu kingine kizuri unastahiki kupokea madoido.

Miungano ya rilei

Miungano ya rilei ni mashirika huru yanayoendesha rilei katika mtandao wa Tor.

Relay mbovu

Jifunze jinsi ya kutoa taarifa juu ya relay ambazo hazifanyi kazi vizuri au zinazoharibu muunganisho wa watumiaji wetu

Maswali ya Kisheria yanayoulizwa mara kwa mara kwa wahudumu wa rilei za Tor

Maswali yanyoulizwa mara kwa mara iliyoandikwa na Msingi wa Mpaka wa Kielektroniki. Ilisasishwa mwisho Marchi 27, 2020.