Mahitaji ya rilei ya Tor hutegemea aina ya rilei na kipimo cha data wanachotoa.

Ikiwa haukidhi masharti ya kuendesha rilei ya Tor au kiungo cha obfs4, kuendesha proksi ya Snowflake ni njia nzuri ya kuchangia kwa kipimo chako cha data ili kuwasaidia watumiaji kukwepa udhibiti.

Kipimo cha data na Viunganisho

Rilei isiyo ya kutoka inapaswa kuwa na uwezo kushughulikia angalau miunganisho 7000 kwa wakati mmoja. Hii inaweza kulemea vipanga njia vya kiwango cha watumiaji. Ikiwa utaendesha rilei ya Tor kutoka kwa seva (ya kawaida au iliyojitolea) kwenye kituo cha data utakuwa sawa. Ikiwa utaiendesha nyuma ya kipanga njia cha watumiaji wa nyumbani itakubidi kujaribu na kuona ikiwa kipanga njia chako cha nymbani kinaweza kushughulikia au ikiwa kitaanza kufeli. Rilei za kutoka kwa haraka (>=100 Mbit/s) kawaida hulazimika kushughulikia miunganisho mingi zaidi inayofanana (>100k).

Inapendekezwa kuwa rilei iwe na angalau kipimo data cha upakiaji cha 16 Mbit/s(Mbps) na kipimo data cha upakuaji cha 16 Mbit/s (Mbps) inayoweza kutumika kwa Tor.Zaidi ni bora. Mahitaji ya kadiri ya chini ya rilei ni 10 Mbit/s (Mbps). Ikiwa una chini ya 10 Mbit/s lakini angalau 1 Mbit/s tunapendekeza uendeshe kiungo chenye usaidizi wa obfs4. Ikiwa hujui kipimo chako cha data unaweza kutumia http://beta.speedtest.net kuipima.

Trafiki inayotoka kila mwezi

Inahitajika kana kwamba rilei ya Tor iruhusiwe kutumia angalau 100 GByte za trafiki inayotoka nje (na kiwango sawa cha trafiki inayoingia) kwa mwezi. Kumbuka: Hiyo ni takriban siku 1 tu ya trafiki kwenye muunganisho wa 10 Mbit/s (Mbps). Zaidi(>2 TB/mwezi) ni bora na imependekezwa. Kiukweli rilei huendeshwa kwa mpango ambao haujapimwa au inajumuisha 2TB kwa mwezi au zaidi. Ikiwa una mpango wa mita unaweza kutaka kusanidi tor kutumia tu kiwango fulani cha kipimo cha data au trafiki ya kila mwezi.

Anwani ya IPv4 ya umma

Kila rilei inahitaji anwani ya IPv4 ya umma - ama moja kwa moja kwa mwenyeji (inayopendelewa) au kupitia NAT na usambazaji wa mlango.

Anwani ya IPv4 haihitajiki kuwa tuli lakini anwani za itifaki wa mtandao zilizo tuli zinapendelewa. Anwani yako ya IPv4 inapaswa kusalia bila kubadilika kwa angalau masaa 3 (ikiwa inabadilika mara kwa mara zaidi ya hapo, haileti maana kubwa kuendesha rilei au kiungo hapo kwani inachukua muda kusambaza orodha mpya ya Itifaki wa mtandao za rilei kwa wateja - ambayo hufanyika mara moja tu kila saa).

Muunganisho wa ziada wa IPv6 ni mzuri na umependekezwa/unahimizwa lakini si sharti. Hakupaswi kuwa na shida ata kidogo na hitaji hili (seva zote zinazopatikana kibiashara huja na angalau anwani moja ya IPv4).

Kumbuka: Unaweza tu kuendesharilei nane za Tor kwa kila anwani ya umma ya IPv4. Ikiwa unataka kuendesha zaidi ya rilei nane utahitaji anwani za IPv4 ziada.

Mahitaji ya Kumbukumbu

  • Rilei isiyo ya kutoka ya <40 Mbit/s inapaswa kuwa na angalau 512 MB ya RAM inayopatikana.
  • Rilei isiyo ya kutoka kwa kasi zaidi ya 40 Mbit/s inapaswa kuwa na angalau 1GB ya RAM.
  • Katika rilei ya kutoka tunapendekeza afadhali 1.5GB ya RAM kwa kila tukio ya Tor.

Hifadhi ya diski

Tor haihitaji hifadhi nyingi ya diski. Rilei ya kawaida ya Tor inahitaji chini ya 200MB kwa data inayohusiana na Tor (pamoja na mfumo wa uendeshaji wenyewe).

CPU

  • CPU yoyote ya kisasa inapaswa kuwa sawa.
  • Inapendekezwa kutumia CPU zilizo na usaidizi wa AESNI (ambayo itaboresha utendakazi na kuruhusu hadi ~ 400-450 Mbps katika kila upande kwenye mfano mmoja wa CPU za kisasa). Ikiwa faili /proc/cpuinfo ina neno aes CPU yako ina msaada kwa AES-NI.

Wakati wa juu

Tor haina hitaji gumu la wakati wa juu lakini ikiwa rilei yako haifanyi kazi kwa zaidi ya masaa 2 kwa siku manufaa yake ni mdogo. Kiukweli rilei huendeshwa kwa seva inayoendeshwa 24/7. Kuwasha tena na kuanzisha tor kikatili ni sawa.

Toleo ya Tor

Kwa sababu za usalama, rilei za Tor hazipaswi kushusha toleo lao la tor kutoka kwa toleo la tor linalosaidiwa hadi toleo lisilosaidiwa la tor. Matoleo mengine ambayo hayajasaidiwa yana ukosefu wa usalama. Huelezea kuwa jaribio la kushusha kwa toleo la ukosefu wa usalama litakataliwa kutoka kwa mtandao wa kiotomatiki.

Kwa muhtasari

Rilei ya kiungo:

  • Angalau 1 Mbit/s ya bandwidth ya juu na chini ya mkondo.

Rilei ya ulinzi/kati:

  • Inaweza kushughulikia angalau miunganisho 7000 ya wakati mmoja.
  • Kuwa na angalau 10 Mbit/s (16 Mbit/s inapendekezwa) ya kipimo data cha juu na chini ya mkondo.
  • Lazima uweze kuchangia angalau 100 GByte za trafiki kwa mwezi (bora 2 TB au zaidi).
  • Angalau 512 MB ya RAM ikiwa rilei ni ya polepole kuliko 40 Mbps au 1 GB ya RAM ikiwa ni kasi zaidi ya 40 Mbps.
  • Anwani ya IPv4 (inaweza kuwa na nguvu au tuli (inayopendelewa) mradi tu ibaki sawa kwa angalau saa 3).
  • Angalau 200 MB ya hifadhi ya diski.
  • Saa inayofaa zaidi ni 24/7 lakini rilei zinapaswa kuwa juu kwa zaidi ya saa 2 kwa siku.

Rilei ya kutoka: Mahitaji sawa ya rilei ya ulinzi/kati plus

  • Angalau 1.5GB ya RAM inapendekezwa.
  • Inapaswa kuwa na uwezo wa kushughulikia miunganisho ya wakati mmoja 100,000 ikiwa ni haraka kuliko 100 Mbit/s.
  • Katika nafasi ya kushughulikia notisi za kisheria na uchunguzi unaowezekana wa kutekeleza sheria. Usiendeshe rilei yako ya kutoka nyumbani kwako.