KUMBUKA: FAQ ni kwa ajili ya taarifa pekee na haijumuishi na msaada wa kisheria. Lengo letu ni kutoa maelezo ya jumla ya masuala ya kisheria yanayoihusu Tor nchini Marekani. Utofauti wa hali halisi na utofauti wa mamlaka kisheria hutoa majibu tofauti kwa maswali kadhaa. Kwa hivyo, unaombwa usichukue hatua pekee yako na habari hii; ukiwa na tatizo lolote la kisheria, suala au maswali pata maelezo kamili kuhusu linalokukumba kutoka kwa wakili aliyesajiliwa kuhudumu kwenye eneo lako.

Pia, ikiwa ulipokea waraka huu kutoka mahali popote isipokuwa tovuti ya EFF au https://community.torproject.org/sw/relay/community-resources/eff-tor-legal-faq, inaweza kuwa imepitwa na wakati, Fuatisha anwani hii kupata toleo jipya.

Je una taarifa ya DMCA? Angalia yetu sample response letter!

Taarifa zote

Je, kuna mtu yeyote amehawahi kushitakiwa au kufunguliwa mashitaka kwa kutumia Tor?

Japokuwa hatujui mtu anashitakiwa, kushitakiwa, au kuweka hatiani kwa kutumia Tor relay, watekelezaji wa sheria katika nchi ya Marekani na nchi zingine mara kwa mara wamechunguza watu kimakosa wanapotumia Tor relay. Tunaamini uendeshaji wa rilei ya Tor, ikijuimisha rilei ya kutoka inayakubalia watu kutuma na kupokea nyendo bila kujilikana, ni haki chini ya sheria xa Marekani.Utekelezaji wa sheriaoften misunderstands jinsi Tor hufanya kazi na mara kwa mara kuhusisha myendo haramu kwenye mtandao kuwa asili yake ni rilei ya Tor ya kutoka. Hii imesababisha polisi kushuku wahudumu wa rilei ya Tor kwa uhalifu na wakati mwingine seizing computer vifaa ikujumuisha rilei za Tor. Kwa mfano, Mwaka 2016 Seattle police mistakenly raided nyumba ya mwanaharakati wa faragha anaye endesha Tor exit relay. Mamlaka za Russian walimkamata kimakosa mwalimu wa hesabu na muendeshaji wa Tor relay Dmitry Bogatov, ingawa baadae walimwachia charges.

Je, nitumie Tor au kuhimiza matumizi ya Tor kwa madhumuni haramu?

Hapana. Tor imetengenezwa kuwa kifaa cha uhuru wa kujieleza, faragha, na haki za kibinadamu. Si kifaa kilichoundwa au kilichokusudiwa kutumika kuvunja sheria, iwe kwa watumiaji wa Tor au waendeshaji wa Tor relay.

Je, EEF zinaweza kuahidi kwamba sitapata tatizo la kuendesha Tor relay?

Hapana. Teknolojia zote mpya zitatengeneza kutokuwa na uhakika wa kisheria, na Tor haitabagua. Hatuwezi kukuhakikishia kuwa hutawai kabiliwa na dhima ya kisheria kutokana na matokeo ya kuendesha rilei ya Tor. Hata hivyo, EFF inaamini kwa uthabiti kwamba wale wanaotumia relay za Tor hawapaswi kuwajibika kwa usarishwaji wa data unaopita katika relay kwa kuwa tunatumia middle relay ya kwetu.

Je, EFF itaniwakilisha ikiwa nitapata tatizo ya kutumia Tor relay?

Ladha. Ingawa EEF haiwezi kuahidi uwasilishi wa waendeshaji wa Tor relay, itasaidia waendesha relay kuifikia hali na itajaribu kutafuta wakili aliyehitimu inapobidi. Maswali kwa EFF kwa madhumuni ya kupata uwakilishi wa kisheria au marejeo yanapaswa kutumwa kwa mratibu wetu wa maingizo kwa kutuma barua pepe kupitia info at eff.org. Maswali kama hayo yatahifadhiwa kwa usiri kulingana na mipaka ya wakili/mapendeleo ya mteja. Kumbaka ingawa EFF haiwezi kutekeleza sheria nje ya Marekani, Itaendelea kujaribu kusaidia waendeshaji wa relay nje ya Marekani katika kutafuta uwakilishi wa ndani.

Je, nitafanyaje ili kupata ziara/kushika mhalifu/mahojiano na polisi?

Ikiwa unazuiliwa na kuhojiwa na polisi, una haki ya kuomba kuongea na wakili kabla na wakati wa kuhojiwa. Ni njia nzuri kusema "Ninataka wakili wangu na ninachagua kubaki kimya" na kisha ukatae kuhojiwa hadi upata nafasi ya kuzungumza na wakili.

Hata hivyo, Ukiamua kuachilia haki yako chini ya usaidizi wa wakili na kujibu maswali bila wakili kuwepo, hakikisha umesema ukweli. Kusema uongo kwa watekelezaji wa sheria kunaweza kusababisha matatizo zaidi kuliko chochote walichotaka kuongea na wewe kabla.

Je, sheria ya Marekani inatoa ulinzi wowote kwa mtandao wa Tor dhidi ya kesi za madai?

Ndio. Sheria ya shirikisho, 47 U.S.C § 230, (mara kwa nyingi huitwa Sehemu ya 230), hutoa kinga ya kisheria kwa wapatanishi wa mtandaoni ambao husimamia au kuchapisha upya hotuba. Ingawa kuna ubaguzi muhimu kwa uhalifu na madai ya miliki ya mali msingi, fungu 230 hukinga huduma za mtandaoni, kama vile mfumo mtandao wa Tor dhidi ya baadhi za sheria ambazo zinaweza kutumika kisheria kukufanya uwajibike kwa kile unachosema na kutenda. Sheria nyingine ya shirikisho, 17 U.S.C. § 512(a), sehemu ya Sheria ya Milenia ya Hakimiliki kidijitali, hutoa usalama wa kushukiwa dhidi ya madai ya ukiukwaji wa hakimiliki kulingana na nyenzo ambazo husambazwa bila kufanyiwa marekebisho, kama Tor relay inavyofanya.

Je, niwasiliane na wasanidi wa Tor nikiwa na maswali ya kisheria kuhusu Tor au niwajulishe ikiwa ninashuku Tor imetumiwa kwa matumizi haramu?

Hapana. Wasanidi Tor's wanapatikana kujibu maswali ya kiufundi, lakini sio wanasheria na hawawezi kukupatia ushauri wa kisheria, wala hawana uwezo wowote wa kuzuia shughuli haramu inayoweza kutokea katika relays za Tor. Zaida ya hayo, mawasilaino yako na watengenezaji wa Tor hayalindwi na upendeleo wowote wa kisheria, kwahiyo utekelezaji wa sheria au washitakiwa wa madai wanaweza kupata taarifa yoyote utakayowapatia.

Unaweza kuwasiliana na info@eff.org ukikumbana na changamato maalum za kisheria. Tutajaribu kukusaidia lakini tukizingatia saizi ndogo ya Msingi wa Mpaka wa Kielektroniki hatuwezi kukuhakikisha tunaweza saidia kila mtu.

Je, watengenezaji wakuu wa Tor's hutoa ahadi yeyote kuhusu uaminifu au kutegemea relays za Tor ambazo zimeorodheshwa kwenye saraka yao?

Hapana. Ingawa wasanidi wa programu wanajaribu kuthibitisha kuwa Tor relay zimeorodheshwa katika saraka zilizodumishwa na wasanidi wakuu ni thabiti na zina kipimo cha data cha kutosha, wao wala EFF hawawezi kuhakikishia uaminifu wa kibinafsi au kutegemewa kwa watu binafsi wanaoendesha relay hizo. Wasanidi wakuu wa Tor wanahifadhi haki ya kukataa ombi la mwendeshaji wa rilei za Tor kuorodheshwa katika saraka au kutoa rilei kutoka kwa saraka yao kwa sababu yoyote ile.

Ondoka katika Relays

Exit relays huongeza wasiwasi kwa sababu usashirishaji wa data kutokea unaweza kutoka na kurudi nyuma katika anwani ya IP ya relay. Ingawa tunaamini kuendesha rilei za kutoka ni halali, ni vigumu mno kwa vitendo kuzuia utumiaji wa rilei za kutokana na shughuli haramu. Hilo linaweza kuwavutia walalamishi wa binafsi watekelezaji wa sheria. Exit relay inaweza kusogeza mbele usafirishaji wa data ambao unashukiwa ipo kinyume cha sheria, na data hiyo inaweza kuhusishwa na mwendeshaji wa relay. Kwa uhakika, polisi wamehusisha kimakosa na usafirishwaji wa data kutoka kwa exit relay kuwa inatoka kwa muendeshaji wa relay's. Kama haupo tayari kukabiliana na hatari hiyo, bridge au middle relay zinaweza kuwa nzuri kuzitumia. Rilei hizi hazisafirishi trafiki kwenye mtandao basi haziwezi kuchanganywa kuwa chanzo cha kinachodaiwa kuwa maudhui haramu.

Blogi ya Tor Project ina baadhi ya [mapendekezo bora] (https://blog.torproject.org/blog/tips-running-exit-node) kwa kuendesha ya kutoka kwa hatari kidogo iwezekanavyo. Tunapendekeza upitie ushauri kabla ya kupangilia rilei ya kutoka.

Je, ninaweza kutumia exit relay kutokea nyumbani kwangu?

Hapana, hii ni hatari na haifai. Ikiwa watekelezaji wa sheria watavutiwa na usafirishaji wa data kutoka katika exit relay yako, Kuna uwezekano kuwa maafisa watahusisha kimakosa usafirishaji wa data huo kama unatoka nyumbani kwako. Hii inaweza sababisha wanaotekeleza sheria kuvamia nyumba yako, kuchukua kompyuta yako na ukawa mshukiwa wa uhalifu. Kwa sababu hiyo, njia bora si kutumia exit ralay nyumbani kwako au kutumia mtandao wako wa nyumbani.

Kutokana na hatari hizi, unapaswa kuzingatia kutumia exit relay yako katika majengo ya kibiashara zinazoendana na Tor. Zina anwani za IP zilizotengenishwa kwenye exit relay yako, na usipitishe usafirishaji wa data kupitia hiyo.

Ukweli kabisa, unapaswa kuepuka kuhifadhi taarifa yeyote nyeti au binafsi kwenye kompyuta iliyohifadhi exit relay yako, na kamwe hupaswi kutumia mashine hiyo kwa madhumuni haramu yeyote. Ikiwa umeamua kutumia exit relay kutoka nyumbani kwako licha ya hizi hatari, tafadhari pitia mapendekezo ya Tor's, ikijumuisha kumwambia ISP wako na kupata anwani tofauti ya IP kwa exit relay.

Je nimwambie ISP wangu kuwa ninatumia exit relay?

Ndio. Hakikisha una urafiiki na ISP wa Tor anayejua unatumia exit relay na atakusaidia katika hilo lengo. Hii itahakikisha kuwa uafikiaji wako kwa mtandao hauzuiliwi kwa malalamiko ya utumizi mbaya. Jumuia la Tor linahifadhi orodha ya watoaji huduma wa mtandao walio na ujuzi wa Tor na pia wasio kuwa nayo.

Je, ni wazo zuri kuwajulisha wengine kuwa ninatumia exit relay?

Ndio. kuwa wazi iwezekanavyo kuhusu ukweli kuwa unatumia exit relay. Ikiwa usafirishwaji data wa kutoka utavutia umakini wa serikali au chama binafsi kisichoridhika, unapaswa watambue haraka na kwa urahisi kuwa wewe ni sehemu ya mtandao wa Tor na huwajibiki kwa maudhui yaliyomo. Hii inaweza kuwa tofauti ya kompyuta yako kuchukuliwa na wanaotekeleza sheria au kutochukuliwa.

Tor project inapendekeza njia zifuatazo kuwajulisha wengine kujua unatumia exit relay:

  • Sanidi jina la nyuma la DNS kwa anwani ya IP ambayo inaweka wazi kuwa kompyuta ni exit relay.
  • Weka notisi kama hii kuelezea kuwa unatumia exit relay kama sehemu ya mtandao wa Tor.
  • Kama inawezekana, pata usajili wa ARIN kwa exit relay yako ambayo huonesha taarifa za mawasiliano yako, sio ya mtoa huduma wako wa mtandao. Kwa njia hii, utapokea malalamishi kuhusu matumuzi mabaya na unaweza kujibu moja kwa moja. Kama sivyo, jaribu kuhakihisha kuwa mtoa hudumu ya mtandao yako anasambaza malalamiko kuhusu matumuzi mabaya inayopokea kwako.

Je, nichunguze usafirishaji wa maandishi ya wazi ambayo hutoka kupitia Tor relay yangu?

Hapana Unaweza kuwa na uwezo wa kiufundi wa kurekebisha vyanzo vya msimbo wa Tor au kusanikinisha programu ya zaida ili kufuatilia au kuweka maandishi ya wazi ambayo yataondoa relay yako. Hata hivyo, waendeshaji wa Tor relay wa Marekani wana uwezekano wa kutengeneza dhima ya kiraia hata ya kijinao ya kwao wenyewe chini ya sheria ya jamhuri au shirikisho la watumia teknolojia ikiwa watafuatilia, kuinga, au kuiba mawasiliano ya watumiajia wa Tor, ilihali waendashaji wasio wa kimarekani wanaweza kuwa chini ya sheria sawa. Usichunguze mawasiliano ya mtu yeyote bila kuzungumza kwanza na mwanasheria.

NIkipokea wito au ombi la maelezo mengine kutoka kwa watekelezaji wa sheria au mtu yeyote anayehusiana na Tor relay yangu, nifanye nini?

Wafundishe kuhusu Tor. katika hali nyingi, usanidi sahihi wa Tor relay hautakuwa na data muhimu kwa wahusika waliouliza, na unapaswa kujisikia huru kuwaelimisha katika muktadha huu. Hadi kiwango unachodumisha kumbukumbu, hufai kuarifu mhusika wa tatu bila kushauriani na wakili. Nchini Marekani, Data hulindwa na Electronic Communications Privacy Act na waendeshaji wa relay nje ya Marekani wanaoweza kuwa chini ya sheria sawa za ulinzi wa data.

Unaweza pokea uchunguzi wa kisheria inayokuzuia kuambia yeyote kuhusu ombi hili. Tunaamini, angalau nchini Marekani, kunyimwa ruhusa ya kujieleza haikuzui kuzungumza na wakili ikijumuisha kupigia wakili upate uwakilishaji. Maswali kwa EFF madhumuni ya kupata uwakilishi wa kisheria yaelekezwe kwa mratibu wetu wa maingizo (info at eff.org). Maswali kama hayo yatahifadhiwa kwa usiri kulingana na mipaka ya wakili/mapendeleo ya mteja.

Kwa taarifa zaidi kuhusu kujibu malalamiko ya unyanyasaji na maswali mengi, Angalia Tor Abuse FAQ na mkusanyiko wa abuse response templates katika tovuti ya Tor Project's.

Kwa taarifa cha nini cha kufanya ikiwa utekelezaji wa sheria unatafuta ufikiwaji wa vifaa vyako vya kidigitali, angalia muongozo wa EFF's Jua haki zako.

ISP wangu, chuoni, n.k amenitumia notisi ya DMCA. Nifanye nini?

EFF imeandika Kiolezo kifupi] ili iweze kukusaidia kuandika majibu kwa mtoa huduma wako wa mtandao, chuoni, n.k, ili kuwafahamisha kuhusu maelezo ya kushukiwa dhidi ya Sheria ya Milenia ya hatimiliki ya kidigitali , na jinsi Tor inavyofaa. Kumbuka kuwa kiolezo kinarejelea mamlaka ya Marekani pekee, na imekusudiwa kudhughulikia malalamiko ya hatimiliki ambayo zinatokana na relay zinazodaiwa kukiuka nyenzo kupitia node ya Tor.

Kama utapenda, utazingatia kutumia nakala ya notisi yako kwa Lumen Database. Barua pepe ya mawasiliano ni team@lumendatabase.org. Hii itatusaidia kutambua mitindo na masuala mawakili wanaweza taka kutazamia. Lumen inahimiza mawasilisho kutoka kwa watu nje ya Marekani pia.

EFF huamini kuwa relay za Tor zinapsawa kulindwa dhidi ya dhima ya hatimiliki kwa vitendo vya watumiaji kwa sababu mwendeshaji wa Tor relay anaweza kuongeza ulinzi chini ya kifungu 512 cha DMCA pamoja na utetezi chini ya mafundisho ya hatimiliki la daraja la juu. Hata hivyo, hakuna mahakama inayoshughulikia masuala haya katika muktadha wa Tor yenyewe. Kama huna raha na kutokuwa na uhakika huu, unaweza kuzingatia kutumia sera iliyopunguza na kuondoka (Kama sheria iliyozoeleka iliyopendekezwa na Tor project) kujaribu kupunguza aina ya usafirishaji wa data ambazo mara kwa mara hulengwa katika malalamiko ya hatimiliki.

Ikiwa wewe ni muendeshaji wa Tor relay na upo tayari kusimamia na kusaidia kuweka mfano wazi wa kisheria uliothibitishwa kwamba kutumia relay hakuleti dhima ya hatimilika kwa waendeshaji au watoa huduma ya kiwango cha data, EFF ingependa kusikia kutoka kwako.

Kiolezo ya majibu ya mwendeshaji wa rilei ya Tor kwa mtoa huduma wa mtandao

Umepata notisi ya Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali? Angalia sampuli yetu ya barua ya majibu!