Unaweza pata fulana ya mikono ya Tor kwa kuchangia kwa mradi wa Tor. Kuna njia mbili kuu ya kuchangia:

  • Tekeleza upeanaji wa haraka wa Tor ambao umekuwa ukifanya kazi kwa miezi miwili iliyopita: unastahiki ikiwa utaruhusu kutoka kwenye bandari la 80 na wastani ya trafiki ni 250 Kilobaiti/sekunde kama si ya kutoka lakini wastani ya trafiki ni 500Kilobaiti/sekunde.

  • Saidia kwa njia nyingine. Dumisha tafsiri. Endesha mafunzo ya Tor. Andika programu nzuri ya usaidizi na upate watu wengi waitumie. Fanya utafiti ya Tor na kutojulikana, tatua baadhi ya hililafu zetu ama ujiimarishe kama mtetezi wa Tor.

Kama unaendesha rilei ya haraka au umefanya kitu kingine kizuri, wasiliana nasi kwa njia ya baruapepe tshirt@torproject.org na maelezo. (Tunataka kuhakikisha shati zetu zinasaidia uhamasishaji kufanyika duniani kote, kwa hivyo tafadhali elewa ikiwa hatuwezi tuma shati tano kwa rilei zako bora.)

Kuna aina mbalimbali za rangi, maumbo na saizi inayopatikana katika muundo mzuri wa mizizi ambao Leiah Jansen alitutengenezea pamoja na miundo ya zamani.