Relay mbovu ni nini?

Relay mbovu ni ile ambayo haifanyi kazi vizuri au inaharibu muunganiko na watumiaji wetu. Hii inaweza kuwa kupitia programu hatarishi au isiyo sanidiwa vizuri. Je ulipata uwasilishaji iliosanidiwa kimakosa, programu hatarishi, au relay yenye mashaka wakati unatumia Tor? Tafadhali tujulishe kwa kututumia barua pepe katika bad-relays AT lists DOT torproject DOT org. Relay nyingi mbovu zimenaswa tunashukuru kwa jamii yetu kuendelea kukua, hivyo shukrani nyingi kwa wote waliotusaidia na kutuangalizia. Maelezo ya relay mbovu pamoja na vigezo vya kuikataa vinapatikana katika [ Network Health wiki.

Pia, kama relay yako ikiwa imeibiwa au imepotea, tafadhali toa taarifa, ili tuweze kuizuia iwapo kuna yeyote aliyeichukua atairudisha mtandaoni.

Zifuatazo kwa sasa zimeruhusiwa japo bado tuna mazungumzo ya kukatazwa (kwa hivyo, hazipaswi kutolewa taarifa kwa wakati huu):

  • Inaruhusu usafirishaji wa maandishi-wazi (kwa mfano, just port 80). Hakuna sababu nzuri ya kutoruhusu data ya mwenza aliyesimbwa (kama port 443), huzifanya relay hizi kuwa mtuhumiwa wa kunusa usafirashaji wa data. Angalia context and spec.

Je, ninawezaje kutoa taarifa juu ya relay mbovu?

Kama umeshakutana na relay mbovu tafadhari tujulishe na andika katika bad-relays AT lists DOT torproject DOT org.

Unaweza kuangalia njia ya kutoka unayoitumia muda wowowte unapotembelea tor check. Tafadhari jumuisha yafuatayo katika taarifa yako:

  1. Anwani ya IP ya relay au fingerprint. Fingerprint ni alama-arobaini katika muundo wa hex kama 203933ED4E55EF8A3C3518427D1A1ED6A4CC285E.
  2. Ni tabia zipi unaziona?
  3. Nyongeza yeyote ya taarifa tutazihitaji kuzalisha suala hilo.

Kama, unahitaji msaada kuhusu chochote kinachohusiana na Tor, tafadhari tumia Jukwaa la Tor inapowezekana.

Nini kinatokea kwenye relay mbovu?

Baada ya kutolea taarifa relay na tukathibitisha tutajaribu kuwasiliana na muendeshaji wa relay, Mara chache tunaweza kutatua tatizo hili na kama tukishindwa (au relay ikiwa na mapungufu ya maelezo ya mawasiliano) tutaibainisha na kuzuia kuendelea kutumika.

Tuna aina tatu za thamani ya programu tunaweza kuzitumia:

  • BadExit- hazitumiki kama exit relay (kwa relay ambazo zinaonesha kuvuruga usafirishaji wa data za kutoka)
  • Isiyo sahihi- Hitumiki isipokuwa kuna mpangilio wa AllowInvalidNodes (Moja kwa moja hii inaruhusu matumizi ya kati na rendezvous)
  • Kataa - kuondoa makubaliano kabisa

Ambayo tunaitumia inategemea matokeo ya mfumo huo, na ikiwa bado salama inaweza kutumika katika hali fulani.

Relay yangu inaonesha bendera ya BadExit. Hii ni nini?

Katika masuala yote ambayo hatuwezi kuwasiliana na muendeshaji kutatua jambo hili, kwa hivyo ikiwa relay yako imepungua uwezo kama BadExit tafadhari tujulishe (tazama hapo juu kwa mawasiliano) ili tufanye kazi pamoja kutatua tatizo hili.

Je, unatafuta kwa bidii relays mbaya?

Ndio. Kwa ugunduzi wa masuala ya otomatiki tizama exitmap and sybilhunter.

Wasimamizi wengine ni pamoja na tortunnel, SoaT, torscanner, na DetecTor.