Asante kwa nia yako ya kutusaidia na tafsiri. Juhudi zetu za localization zimeungwa mkono na Localization Lab.

Orodha ya barua pepe ya utafsiri

Kuwasiliana na watafsiri wengine, tafadhali jiunge na Tor localization mailing list, ambapo tunapanga tafsiri, kuchukua maamuzi, kuripoti hitilafu katika alama zinazotambua chanzo cha kutafsiri n.k. Tafadhali jitambulishe na uulize maswali yeyote unayoweza kuwa nayo baada ya kufuata maelekezo haya.

Jukwaa la kutafsiri

Juhudi zetu za localization zimewekwa katika weblate, Jukwaa la utafsiri kwa watu wengine.

You can submit anonymous suggestions, but it is better to create an account so you can comment and discuss with other translators, or review their contributions.

Kumbuka kwamba jina la mtumiaji na anwani ya barua pepe utakayoichagua itaonekana hadharani kwenye mfumo wa tafsiri kwa kuwa yatahusishwa na mabadiliko unayoyafanya. Tunahimiza matumizi ya akaunti bandia.

Kabla ya kutafsiri, tafadhari soma kupitia ukurasa wa Tor Project kwenye Localization Lab Wiki, na nyaraka zetu katika Tor L10n wiki for translators na reviewers. Ukurasa huu unajumuisha miongozo, taarifa, na vipaumbele vitakavyo kusaidia kufaidika kutokana na mchango wako.

Kujisajili kwenye Weblate

  1. Nenda kwenye ukurasa wa kujisajili kwenye wavuti. Kumbuka kwamba jina la mtumiaji na anwani ya barua pepe utakayoichagua itaonekana hadharani kwenye mfumo wa tafsiri kwa kuwa yatahusishwa na mabadiliko unayoyafanya. Tunahimiza matumizi ya akaunti bandia.
  2. Jaza ukurasa unaofuata na maelezo yako, na usubiri barua pepe ya uthibitishaji (inaweza kuchukua hadi dakika 10 kufika kwenye kikasha chako).
  3. Washa akaunti yako kwa kubofya barua pepe kutoka kwa tovuti, kukubaliana na sheria na masharti na kuongeza nenosiri jipya.
  4. Katika ukurasa unaofuata, chagua lugha utakazotafsiri kutoka kwenye menyu, na uhifadhi.
  5. Nenda kwenye Arifa na uchague Mradi wa Tor kutoka kwa miradi inayotazamwa. Miradi mingine tunayoipendekeza ni Guardian Project na Onionshare: Tazama mradi wa Tor katika Weblate.
  6. Make sure to also select notifications for your watched projects.
  7. Sasa utaona tafsiri za Tor Project kwenye dashibodi yako ya tovuti: dashibodi ya weblate.

Nini cha kutafsiri ya kwanza?

Unaweza ona tafsiri kwa kipaumbele zaidi katika ukurasa wetu wa takwimu za tafsiri.

IRC chaneli

Tunabarizi katika chaneli ya #tor-l10n kwenye mtandao wa oftc IRC. Tafadhali jiunge nasi ili kuzungumzia ujanibishaji (l10n)! Unaweza pia kutumia Element https://element.io/ to connect: #tor-l10n:matrix.org.