1. Sakinisha vifurushi vinavyohitajika

apt-get install unattended-upgrades apt-listchanges

2. Sasisha faili ya usanidi

Hii inachukulia kuwa utasanidi hazina ya kifurushi cha Tor Project kwa Debian/Ubuntu, ambayo imeandikwa hapa.

Weka mistari iliyo hapa chini kwenye faili ya usanidi /etc/apt/apt.conf.d/50unattended-upgrades kila kitu ambacho kilikuwa ndani ya faili iliyotengenezwa kinaweza kuondolewa kabla ya kuongeza mistari iliyo hapa chini.

Debian:

Unattended-Upgrade::Origins-Pattern {
    "origin=Debian,codename=${distro_codename},label=Debian-Security";
    "origin=TorProject";
};
Unattended-Upgrade::Package-Blacklist {
};

Ubuntu:

Unattended-Upgrade::Allowed-Origins {
    "${distro_id}:${distro_codename}-security";
    "TorProject:${distro_codename}";
};
Unattended-Upgrade::Package-Blacklist {
};

Debian na Ubuntu

Sasisha faili /etc/apt/apt.conf.d/20auto-upgrades na maudhui yafuatayo

APT::Periodic::Update-Package-Lists "1";
APT::Periodic::AutocleanInterval "5";
APT::Periodic::Unattended-Upgrade "1";
APT::Periodic::Verbose "1";

3. Anzisha upya kiotomatika

Ikiwa unataka kuwasha upya kiotomatiki ongeza yafuatayo mwishoni mwa faili /etc/apt/apt.conf.d/50unattended-upgrades:

Unattended-Upgrade::Automatic-Reboot "true";

4. Tahini

Unaweza kujaribu usanidi wako wa uboreshaji ambao haujashughulikiwa na amri ifuatayo:

# unattended-upgrade --debug

Ikiwa unataka kuona matokeo ya utatuzi lakini usibadilishe chochote tumia:

# unattended-upgrade --debug --dry-run