Anwani "Batili" za onion ni sehemu ya suluhisho ukiwa na ugumu wa kukariri anwani ndefu za onion zenye 56-char.

Anwani batili ni anwani ya onion ambayo huanza idadi ya alama ambazo zilichaguliwa-awali, kawaida ni jina linalohusiana na Onion Service maalum.

Kwa mfano, mtu anaweza kujaribu kutoa anwani ya onion kwa tovuti ya mysitename na akaishia na kitu kinachoonekana kama hiki:

mysitenameyx4fi3l6x2gyzmtmgxjyqyorj9qsb5r543izcwymle.onion

Hii ina faida kiasi:

  • Ni rahisi kwa watumiaji wa Onion Services kujua ni tovuti ipi ambayo wanakaribia kuifikia.

  • Ina mvuto wa chapa kwa wamiliki wa tovuti.

  • Ni rahisi kwa waendesha Onion Services kutatua dosari na kujua huduma ipi ina makosa bila kurudia kwenye jedwali au kukumbuka baadhi ya alama mchanganyiko kutoka katika anwani ya kawaida ya onion.

Lakini pia ina baadhi ya hasara:

  • Mshambuliaji anayetaka kuiga onionsite iliyopo kwa kuunda toleo la kughushi anaweza kutumia njia ya ziada ya anwani batili kuwashawishi watumiaji kwamba anwani zao ni sahihi. Ikiwa tovuti halali haitumii anwani batili, watumiaji wanaweza kufikiri tovuti ghushi ndio halali na hii kwa sababu ina anwani nzuri zaidi.

  • Ni rahisi kwa mtu yeyote mwenye vitu vichache vya kuchakata kutengeneza funguo zingine zinazoanzia na mysitename(ingawa hakuna uwezekano mkubwa wa kupata funguo halisi kutoka katika mfano hapo juu). Kwa hiyo, inamaananisha, funguo batili zinaweza kutatanisha na kutoa utambulisho usio sahihi, watumiaji wanaweza kukosea kwa urahisi kuiga ufikiaji wa onion service kwa sababu tu inaanza na mysitename.

  • Inagharimu rasilimali (muda na nguvu): jina kubwa batili, ina chukua muda mrefu (na uwezo mkubwa zaidi wa kuchakata).

Suluhisho la muda mrefu linahusisha mpango bora wa kutoa majina ya onion, na mapendekezo yaliyopo, ambayo yatatengeneza majina batili tu kama njia ya kuwasaidia wasimamizi wa mifumo kupanga anwani za onion. Kwa mfano, unapoendeshaOnionbalance nyingi za nyuma.

Utengenezaji wa anwani batili

mkp224o ni alama mojawapo za data zinazo tumika kutengeneza anwani batili.

Hatua ya 1 sanikisha vitu vinavyohitajika

Hatua ya 2 Fuata Maelekezo ya kutengeneza

Hatua ya 3 Bofya generator

$ ./mkp224o -d onions mysitename

Hii itaunda folda jipya onions na folda za kila moja kwa anwani za onion zilizogunduliwa zikiwa na funguo zake husika. Kwa machaguo zaidi, rejea hapa:

$ ./mkp224o -h

Soma zaidi