Waendeshaji waOnion services wanapaswa kufanya mazoezi ipasavyo juu ya ulinzi katika utendaji na usimamizi wa mifumo ili kutunza ulinzi. Kwa mapendekezo baadhi ya usalama tafadhali hakikisha unasoma juu ya Riseup's "Tor Hidden (Onion) Services Best Practices" document. Pia, hapa kuna baadhi ya mambo yasiyojulikana unapaswa kuweka katika akili yako:

  • Kama ilivyotajwa hapa, kuwa mwangalifu usiruhusu seva yako ya tovuti kufichua taarifa inayokutambulisha, kompyuta yako au eneo lako ulipo. Kwa mfano, wasomaji labda wanaweza kuamua ikiwa thttpd au Apache, na kusoma kitu juu ya mfumo wako wa uendeshaji.
  • Kama kompyuta yako haipo mtandaoni muda wote, pia Onion Service yako haitakuwepo. Hii inavujisha taarifa kwa adui mwangalifu.
  • Kwa ujumla hili ni wazo zuri kutumia Onion Service kwa watumiaji Tor badala ya Tor relay, kwa kuwa muda wa relay na shughuli zingine zinaonekana hadharani.
  • Kadri Onion Service zinapofanyika kwa muda mrefu mtandaoni, hatari ni kubwa zaidi hugundulika katika hilo eneo. Mashambulizi maarufu zaidi ni yale kutengeneza wasifu wa upatikanaji wa Onion Service's na kulinganisha na mifumo usafirishaji wa data katika njia sahihi.
  • Suala lingine la kawaida ni ikiwa utatumia HTTPS kwenye tavuti ya onion au la. Angalia Chapisho hili katika Blog ya Tor na ujifunze zaidi juu ya mambo haya.
  • ili kulinda Onion Service zako kutoka kwa wadukuzi wenye uwezo mkubwa zaidi unapaswa kutumia Vanguards addon, soma read Tor blog about Vanguards and Vanguards' Security README.