Zaidi ya imani potofu na maoni potofu, Utetezi wa Onion Services na kuimarisha teknolojia ya faragha mara zingine huwa ni changamoto. Kuna masuala tofauti ya matumizi, na kuwafikia watu muhimu katika masuala maalum ya matumizi badala ya nyingine, unaweza kuwahusisha na kuwaongoza katika huduma mpya za onion katika mpangilio.

Hoja hizi za mazungumzo zitasaidia kuelezea jinsi Onion Service hutoa faida nyingi za faragha na usalama katika muktadha tofauti.

  • Jinsi gani Onion Services inafanya kazi
  • Uhuru wa vyombo vya habari na ukwepaji wa udhibiti
  • Uendelevu wa mtandao
  • Ongeza kiwango cha faragha katika huduma zako
  • Linda vyanzo, watoa taarifa , na waandishi wa habari
  • Gawanya kulingana na
  • Waelimishe watumiaji juu ya faragha ya kubuni
  • Kusumbua au kuondoa Metadata

Jinsi gani Onion Services hufanya kazi

Mtumiaji muhimu pengine tayari kasikia kuhusu Tor Project, Mtandao na pengine realays za Tor, na hiyo ni nzuri! Tor relays ni sehemu ya miundombinu ya umma, ambapo usafirishaji wa data uliosimbwa kwa watumiaji wa Tor hupitishwa kufikia ili kufikia mtandao huru. Onion services si kama Tor relay katika mtandao.

Onion Service katika mtandao wa Tor hujifanya kama mtumiaji mwingine wa Tor. Onion Service ili iweze kupatikana katika mtandao unganisha kwenye nodi za rendezvous. Mtumiaji anayetaka kufikia Onion Service vivyo hivyo.

Hii inaamaanisha kuwa muunganiko kutoka kwa mtumiaji hadi kwenye seva hauachi kamwe mtandao wa Tor. Katika utofauti wa kutumia Tor relay, kutumia Tor Onion Service haisababishi majibu ambayo anwani yako ya IP kuorodhesha hadharani popote, wala huduma yako ya relay haileti Tor ingine.

Kwa uelewa mkubwa, soma Mapitio ya OnionServices na tizama mazungumzo haya: DEF CON 25 - Next Generation Tor Onion Services.

Uhuru wa vyombo vya habari na kukwepa udhibiti

Muunganiko wa kawaida wa Tor tayari umetoa ukwepaji wa udhibiti, lakini Onion Service pekee unaweza kuficha pande zote za mawasiliano kati ya - mtumiaji na mtoa huduma -, hutengeneza mawasiliano huru ya metadata kati ya mtumiaji wa huduma na huduma yenyewe.

Teknolojia ya udhibiti huwa inasambazwa na wadau mbalimbali, kama serikali na watoa huduma za mtandao, duniani kote ili kuzuia ufikiwaji katika uhuru wa habari na faragha ya vifaa.

Ili kulinda uhuru wa kujieleza na uhuru wa mawazo katika nafasi zilizodhibitiwa, mashirika makubwa ya vyombo vya habari yamefanya tovuti zao kupatikana katika Onion Services kwa miaka michache iliyopita.

Haya ndiyo masuala ya NY Times, ProPublica, Deutsche Welle, BBC, The Markup na vyumba vingine vya habari.

Mradi wa Usalama wa habari, ulianzishwa na Uhuru wa vyombo vya habari, hufuatilia jinsi ya kulinda taarifa za tovuti za masharika ya habari ni. moja ya vipimo vya kupitishwa kwa Onion Services.

Soma taarifa za matangazo ya mashirika juu ya tovuti zao za onion:

  • "Tulizindua hili kwa sababu tunaripoti sana, kuandika, na kusimba juu ya mambo kama udhibiti wa vyombo vya habari, ufalitiaji wa faragha ya kidigitali, na ukiukaji wa taarifa za kibinafsi za matibabu. Wasomaji hutumia hifadhi data zetu zinazolingana kuangalia taarifa zilizofichwa juu yao, kama vile daktari amepokea malipo kutoka makampuni ya madawa. Wasomaji wetu hawapaswi kuhofu kuwa kuna mtu mwingine anamwangalia nini anafanya katika tovuti yetu. Kwa hiyo tulifanya tovuti yetu ipatikane kama huduma iliyofichwa ya Tor (Onion Service) ili kuwapa wasomaji njia ya kuvinjari tovuti yetu huku akiacha njia chache za kidigitali."ProPublica

  • "Baadhi ya wasomaji huchagua kutumia Tor ili kupata uandishi wetu kwa sababu huzuiwa kitaalamu kufikia tovuti yetu, au kwa kuwa huhofia udhibiti wa mtandao wa ndani ya nchi husika, au kwa sababu hujali juu ya faragha ya mtandaoni, au kwa sababu hiyo ndiyo njia wanayoipendelea." [Majira ya New York]New York Times

  • "DW ni mtetezi wa kimataifa wa uhuru wa maoni na uhuru wa kujieleza. [...] kwa hiyo ni hatua ya kimantiki kwa sisi pia kutumia Tor ili kuwafikia watu kaatika masoko yaliyodhibitiwa ambao hapo awali walikuwa na ufikiwaji kwa kiwango kidogo au hakuna ufikiwaji wa vyombo vya habari bila malipo." Deutsche Welle

  • "Kivinjari kinaweza kuficha nani anayekitumia na data gani inafikiwa, ambayo inaweza kuwasaidia watu kuepuka ukwepaji wa udhibiti wa mtandao kutoka serikalini, Nchi kama China, Iran na Vietnam ni miongoni mwa nchi zilizojaribu kuzuia ufikiwaji wa tovuti ya habari ya BBC au vipindi vyake." BBC

Uendelevu wa Mtandao

Muingiliano wa mawasiliano unaozalishwa na Onion Services hauachi mtandao wa Tor, na hivyo, sakiti hizi onion huweka huru kipimo cha relay ya kutoka kwa wengine. Hii ni muhimu kwa sababu relay za kutoka ni vyanzo vichache, vinavyo tengeneza 20% tu ya relay 7000. Kama vile wao ni sehemu ndogo ya mtandao, kwa kawaida, exit relay zinajaa kupita kiasi na kuwakilisha kizuizi kwa uzoefu wa kuvinjari kwa watumiaji wa mtandao wa Tor.

Onion services haitumii njia hiyo hiyo ya sakiti kama viunganishio vya kawaida vya Tor. Wakati huduma inapatikana katika Onion Services, inaongeza utofauti katika mtandao wa Tor kwa sababu hutumia mpangilio tofauti wa sakiti katika mtandao, kuepuka relays za kutoka kabisa. Kama matokeo ya muundo huu, Onion Services na watumiaji wake wana kinga dhidi ya mashambulizi yanayohusiana na bad exit relays.

Ongeza kiwango cha huduma zako za faragha

Zaidi ya tovuti na tovuti za onion, Ni rahisi kufanya mambo nmengi kupitia Onion Services, kwa mfano, Barua pepe. Japokuwa watumiaji wanaofahamu faragha wanaweza kutumia vifaa vinavyolinda mawasiliano yako kama OpenPGP, Kuna metadata nyingi zilizosimbwa katika barua pepe: kwa mfano nani anayewasiliana nani, lini, mara ngapi, wapi, lini ilitumwa na kupolewa, aina gani ya kompyuta ilitolewa, nk.

Kama Edward Snowden anavyooensha katika kitabu chake, "Permanent Record" (2019),

"Unajua unachokisema wakati unapiga simu, au unachoandika katika barua pepe, Lakini huwezi kuzidhibiti metadata unayoitoa, kasababu hujitengeneza yenyewe otomatiki. [...], Kwa mjumuisho, Metadata inaweza kumwambia mchunguzi wako wa karibu kila kitu anachokitaka au kujua kuhusu wewe, isipokuwa kile kinachoendelea kwenye kichwa chake.

Onionmx ni programu tumizi inayo ruhusu utaoji madhubuti wa barua pepe katika Onion Services, hutatiza metadata ya nani huzungumza na nani. Watoa huduma za barua pepe kama Riseup, Systemlina wengine wengi protect their users privacy using onionmx.

Watoa huduma wengine kama Proton huruhusu watumiaji kusoma na kutuma barua pepe zao kwa usalama na bila kujulikana katika tovuti za mteja wao ambazo hutumika na tovuti za onion.

Linda vyanzo, watoa taarifa, na waandishi wa habari

Waandishi wa habari wengi na makampuni ya utangazaji hutumia vifaa vinavyoendana na Onion Service kulinda vyanzo vyao. Husambaza na kuruhusu nyaraka kutoka katika vyanzo visivyojulikana kwa kutumia vifaa kama SecureDrop, GlobalLeaks au OnionShare.

Hapo awali ulitengenezwa na Aaron Swartz, SecureDrop ni mfumo huria wa uwasilishaji kwa watoa taarifa uliosimamiwa na Uhuru wa Vyombo vya habari na kusambazwa na makampuni mpya mengi duniani kote. Vyanzo vya SecureDrop, hutuma nyaraka pekee katika njia salama isiyojulikana, kwa kutumia Tor Browser. Hivyo, mwandishi wa habari hataweza kujua mwandishi ni nani na hawezi kuweka vyanzo hatarini.

GlobaLeaks ni chanzo huru cha jukwaa la watoa taarifa kilichojikita katika kubebeka na kupatikana. Ni programu ya tovuti inayotumika kama Onion Service ambayo watoa taarifa na waandishi wa habari wanaweza kubadilishana taarifa na mafaili bila kujulikana. Mradi ulioanzishwa mwaka 2011 na kikundi cha waitaliano, sasa unaendelezwa na Kituo cha Hermes cha uwazi na haki za kibinadamu za kidigitali.

OnionShare ni kifaa kingine kulingana na Onion Services kinachotumia uimara wa kutojulikana katika kusambaza mafaili nyeti kati ya waandishi wa habari kwa usalama. Ni rahisi kusimamia mafaili katika kompyuta yako na kuyasambaza (kutuma na kupokea) kwa kutumia Onion Services. Wapokeaji wote wa mawasiliano wanahitaji kusanikisha Tor Browser katika kompyuta zao ili kufungua anwani za onion. OnionShare ilitengenezwa baada ya kukiukwa kwa haki za binadamu mwaka 2013 wakati wa Snowden revelations,

"Kwa mara ya kwanza nilitambua mahitaji ya kifaa hichi nilipojifunza jinsi David Miranda, mshiriki mwenzangu wa Glenn Greenwald, alipozuiliwa kwa maasa tisa pale uwanja wa ndege wa Landon alipokuwa akijaribu kusafiri kuruka nyumbani kuelekea Brazil.
Kufanya kazi ya uandishishi wa habari katika Guardian, Marinda alikuwa ambeba kibebeo cha USB chenye nyaraka nyeti.
Nalijua kuwa ungeweza kutuma nyaraka kwa usalama kwenye mtandao kwa kutumia Tor Onion Service, mojawapo ya teknolojia zisizothaminiwa katika mtandao, na kuepuka hatari za kusafiri pamoja nao.
Nilitengeneza OnionShare ili kufanya mchakato wa kusambaza faili hili katika mtandao wa Tor upatikane zaidi kwa kila mtu." [OnionShare 2 release](https://blog.torproject.org/new-release-onionshare-2)

Gawanya kulinga na

Kama ilivyofafanuliwa katika Mapitio], hakuna mamlaka ya kati inayothibitisha au kukataa Onion Services. Anwani ya Onion Service hutengenezwa kiotomatiki. Waendeshaji hawatumii miundombinu ya kawaida ya DNS na hawahitaji kununua au kusajili jina la kikoa.

Mfano mzuri wa matumizi haya ni programu ya mazungumzo Ricochet Refresh. Ricochet hutumia Onion Services kutengenza usalama wa mawasiliano yenye vipengele hivi, kuzuia metadata, kutojulikana, na mgawanyiko. Katika Ricochet Refresh, Kila mtumiaji ni Onion Service. Na kwa sababu hiyo, hakuna seva ya kati itakayoathiriwa na mshambuliaji.

Elimisha watumiaji kuhusu faragha kwa kubuni

Onion services ni mfano bora wa faragha ya teknolojia ya kubuni, ambapo mtu hulindwa na kutojulikana moja kwa moja. Kufanya huduma zako zikapatikana katika Onion Services ni fursa ya kuelimisha jamii kwa ujumla juu ya Tor na jinsi njia salama zaidi za kufikia mtandao unaoonekana kama: urahisi wa kuvinjari kurasa ya tovuti. Hamasika zaidi na kampeni yetu #MoreOnionsPorFavor na uwafundishe wengine juu ya umuhimu wa kutojulikana.

Usumbufu au uondoaji wa Metadata

Wakati unatumia mtandao wa Tor kuvinjari cha tovuti uliyopo hazitumi taarifa yoyote kwa namna moja au ingine kuwa wewe ni nani na unaunganishwa kutoka wapi. Onion Services hutumia mtandao wa Tor ili kuondoa taarifa kuhusu watumiaji walipo. Kuzitumia huondoa metadata zote ambazo zinaweza kuhusiana na huduma au vinginevyo.

Onion moja kwa siku huzuia ufuatiliaji

Sasa umeshajua manufaa yote ya Onion Services, utahitaji kuweka mpangilio katika tovuti ya onion na kusoma juu ya muhtasari wa mpangilio.