Mwongozo huu unapaswa kufanya kazi kwa matoleo ya hivi karibuni ya mfumo wa uendeshaji wa OpenBSD. Inashughulikia masasisho/maboresho ya vifurushi pekee, na haitumii kiraka kingine chochote kwenye mfumo wa msingi au kernel.

KUMBUKA: Hatua zote zilizoandikwa katika ukusa huu zinazingatia kuwa seva yako imejitolea kutoa rilei ya Tor. Tafadhali fahamu kuwa huduma zitaanzishwa upya wakatu wa mchakato wa kusasisha programu ya kiotomatiki iliyoandikwa hapa.

1. Unda Hati ya Usasisho

OpenBSD inatupa njia rahisi ya kuendesha kazi kila siku, kila wiki au kila mwezi. Inaturuhusu kuandika hati yetu maalum ya kuitwa na cron katika faili tatu tofauti za kawaida (kulingana na mahitaji yetu, au chaguo fulani):

  • /etc/daily.local
  • /etc/weekly.local
  • /etc/monthly.local

Kwa mfano huu tutatumia /etc/weekly.local:

#!/bin/sh
PATH="/bin:/usr/bin:/sbin:/usr/sbin:/usr/local/bin:/usr/local/sbin"
RAND=$(jot -r 1 900)
sleep ${RAND}
pkg_add -u -I && \
rcctl restart tor

Kwa ratiba hii mahususi, tunachagua kuendesha hati kila wiki siku za Jumamosi saa 3h30 (kulingana na saa za eneo lako). Itaanzisha mchakato wa masasisho ya vifurushi yenyewe kulingana na thamani iliyoekwa kwa utofauti wa $RAND. Imesanidiwa kutoa usingizi kati ya sekundi 0 na 900 (dakika 15).

2. Anzisha tena cron

Mwisho anzisha tena cron daemon ili kufanya mabadiliko ya usanidi kutumika.

# rcctl restart cron