Mwongozo huu unapaswa kufanya kazi kwa DragonFlyBSD, FreeBSD, na mfumo wa uendeshaji wa HardenedBSD. Inashughulikia masasisho/maboresho ya vifurushi ONLY na haitumii kiraka kingine chochote kwenye mfumo wa msingi au kernel.

KUMBUKA Hatua zote zimeandikwa katika ukurasa huu zinazingatia kuwa seva yako imejitolea kutoa huduma ya upeanaji wa Tor (kiungo/ulinzi/kutoka). Tafadhali fahamu kuwa services zitaanzishwa upya wakati wa mchakato wa kusasisha programu kiotomatiki ulioandikwa hapa.

1. Unda Hati ya Usasisho

Hebu tutumie /root/bin/pkg-upgrade.sh kwa usanidi wetu. Hivi ndivyo inavyopaswa kuonekana kama:

#!/bin/sh
PATH="/bin:/usr/bin:/sbin:/usr/sbin:/usr/local/bin:/usr/local/sbin"
RAND=$(jot -r 1 900)
ENV="BATCH=yes IGNORE_OSVERSION=yes"
sleep ${RAND}
env ${ENV} pkg update -q -f && \
env ${ENV} pkg upgrade -q -U -y --fetch-only && \
env ${ENV} HANDLE_RC_SCRIPTS=yes pkg upgrade -q -U -y

2. Panga kazi ya cron

Kwa ratiba hii mahususi tunachagua kuendesha hati kila saa 0h00 (kulingana na saa za eneo) na itaanzisha mchakato wa masasisho ya vifurushi yenyewe kulingana na thamani iliyowekwa kwa utofauti wa $RAND - imesanidiwa kutoa kulala kati ya sekunde 0 na 900 (dakika 15).

# echo "0 0 * * * root /bin/sh /root/bin/pkg-upgrade.sh" > /etc/cron.d/pkg-upgrade
  • Ikiwa ungependa kubadilisha utekelezaji ulioratibiwa wa hati ya sasisho sanidi mipangilio ya crontab yako hadi thamani ambayo ungependa kutumia.

3.Anzisha tena cron

Mwisho anzisha tena cron daemon ili kufanya mabadiliko ya usanidi kutumika.

# service cron restart