Panga na jamuiya, mikutano ni njia nzuri ya kupata na kuimarisha jumuiya ya wafuasi wa faragha katika eneo lako.
Hatua 1
Watafutie sehemu ya ndani ya eneo lako ambayo itawaruhusu kukutana kwa lisaa au masaa mawili. Maktaba ya umma, kituo cha kijamii, sehemu wanayokutana wataalam mbalimbali au chumba katika chuo kuu ni baadhi ya maeneo unayoweza kuandaa tukio lako.
Hatua ya 2
Chagua tarehe na muda ambao ni rafiki kwa kikundi chako na eneo la karibu. Mwishoni mwa wiki au katikaki ya wiki, baada ya saa za kazi (7pm) inaweza kuwa nzuri. Baada ya kuthibitisha eneo na tarehe, tengeneza bango na toa mualiko mtandaoni ili kueneza tukio hilo.
Hatua ya 3
Tafuta muwezeshaji wa mkutano na uandike ajenda, kwa mfano, Maswali na majibu juu ya Tor, Jinsi ya kupangilia relays. Soma na fuatisha Utendaji wetu ulio bora.
Hatua ya 4
Kabla ya mkutano, Panga eneo la kufanya tukio. Nunua baadhi ya vitafunio na chips, bandika baadhi ya mabango karibu na eneo la tukio, hii itawasaidia watu kupatafuta kwa urahisi. Kama una baadhi ya taarifa zilizochapishwa na/au vitu vizuri vya Tor, weka juu ya meza.
Hatua ya 5
Andaa wasilisho lako na subiri kwa dakika chache watu wafike. Wakati shughuli inaendelea andika maswali, wangapi wanaijua Tor kabla, wangapi ni waedesha relay, n.k
Hatua ya 6
Baada ya mkutano, safisha eneo, ondoa mabango na tuma madekezo yako kwa Timu ya Jumuiya ya Tor kupitia orodha ya barua pepe.